FM Manyara

Vijana Babati watakiwa kujiepusha na makundi mtandao

12 July 2026, 1:16 pm

Picha ya baadhi ya vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati wakiwa kwenye kongamano la vijana

Vijana katika Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara wametakiwa kutokujihusisha na makundi mtandao ambayo hutumika kuchochoea vurugu na kurudisha maendeleo nyuma.

Na Marino Kawishe

Akifunga kongamano la Vijana la siku moja lililofanyika julai 11, 2026 katika halmashauri ya wilaya ya Babati kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Remidius Mwema Emanuel amesema kuwa jukwaa hilo limewakutanisha vijana pamoja ili kuona ni kwa namna gani changamoto mbali mbali zinazowakabili zinatafutiwa ufumbuzi na kuona  maendeleo yao yanakuwa.

Sauti ya kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Remidius Mwema Emanuel

Nae mkuu wa Idara ya maendeleo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Babati January Bikubwa amewaasa vijana kujifunza kila siku na kufanya kazi kwa nidhamu huku akiwataka kutokulalamikia mazingira. 

Sauti ya mkuu wa Idara ya maendeleo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Babati January Bikubwa
Picha ya mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Remideu Mwema