FM Manyara
FM Manyara
14 May 2026, 4:59 pm

Wanaushirika mkoani Manyara wametakiwa kuendesha shughuli za ushirika kwa kuzingatia uadilifu na kutimiza majukumu yao kama sheria zinavyoelekeza katika usimamizi wa vyama vya ushirika.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa leo na mrajisi msadizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Manyara Absalom Cheliga wakati akiongea katika jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Manyara.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la ushirika mkoa wa Manyara Ramadhani Ismail amesema tangu kuanza kwa jukwaa hilo mkoa wa Manyara umenufaika kutokana na elimu ambayo imekuwa ikitolewa kwa wanaushirika kama inavyoelekezwa katika misingi ya ushirika.

Nao baadhi ya wanaushirika ambao wameudhuria katika jukwaa hilo, wamesema wamenufaika na elimu ambayo imetolewa jinsi ya kuendesha vyama vya misingi pamoja na kuwaelimisha wanachama umuhimu wa vyama vya ushrika.
