FM Manyara
FM Manyara
7 July 2026, 12:34 pm

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani, amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku bila hofu, ikiwemo kusherehekea Sikukuu ya Saba Saba kwa amani, akisema kuwa hadi sasa hakuna kiashiria chochote cha uvunjifu wa amani kilichorekodiwa mkoani humo.
Na Marino Kawishe
Akizungumza na FM Manyara, Kamanda Makarani amesema Jeshi la Polisi limekuwa likijiandaa kikamilifu kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatilia na kudhibiti viashiria vyovyote vya uhalifu vinavyoweza kuhusishwa na wito wa maandamano uliosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa upande mwingine, Kamanda Makarani amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwakamata watu waliohusika na mauaji ya vijana wawili pamoja na uporaji wa pikipiki zao, ambapo vijana hao waliuawa na watu wasiojulikana.