FM Manyara
FM Manyara
20 July 2026, 5:03 pm

Zaidi ya wananchi elfu 8 katika kijiji cha ngeju kilichopo kata ya Namelock wilayani Kiteto mkoani Manyara kunufaika na mnara wa mawasiliano wenye uwezo wa 4G na 5G
Na Marino Kawishe
Kampuni ya simu za mikononi ya Yas na Mixx By Yas Tanzania wamezindua mnara wa mawasiliano wenye uwezo wa 4G na 5G ambao utawanufaisha zaidi ya wananchi elfu 8 katika kijiji cha ngeju kilichopo kata ya Namelock wilayani kiteto mkoani Manyara.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mnara huo mkuu wa kanda ya kaskazini kutoka mtandao huo Robert Sanyagiamesema lengo la kampuni hiyo nikutoa huduma za mawasiliano zitakazowanufaisha wananchi kiuchumi ikiwemo kutoa na kuweka pesa, na kuwasiliana kikamilifu bila kikakwazo cha mtandao.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wamekiri mtandao wa Yas Tanzania utawanufaisha na kutatua kero za mawasiliano ambazo zilikuepo hapo awali kwenye eneo hilo.
Nae Mwenyekiti wa kijiji cha ngeju, Petro Singero amewashukuru viongozi wa kampuni hiyo ya simu za mkononi kwakuona fursa na kuwekeza mnara huo kwenye kijiji hicho ili kuwaondolea changamoto iliyokuwepo kwa muda mrefu ya kimtandao.
Aidha,kuzinduliwa kwa mnara huo wa mawasiliano ya simu za mkononi wa kampuni ya Yas Tanzania kuna fanya mkoa wa Manyara kuwa na zaidi ya minara 100 inayohudumiwa na Yas kwa kutoa huduma kwa wananchi na ambayo imewekeza zaidi ya shilingi Trillion moja hapa nchini na kuwa ni kampuni yenye zaidi ya minara elfu 4800 yenye kasi ya 4G plus mpaka sasa.
