FM Manyara

Teknolojia ya nzi chuma yatajwa suluhisho la changamoto ya taka Manyara

10 June 2026, 5:16 pm

Picha ya baadhi ya washiriki wa Kongano bunifu katika sekta ya maji na usafi wa mazingira (WASH

Kongano bunifu katika sekta ya maji na usafi wa mazingira (WASH) lijulakanalo kama kongano la udhibiti na uchakataji taka Manyara limezinduliwa leo katika mkoa wa Manyara lengo ikiwa ni kuhakikisha taka zote zinakuwa fursa.

Na Mzidalfa Zaid

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara kaimu katibu tawala idara ya huduma za uchumi na uzalishaji  mkoa wa manyara Faraja Ngelageza amesema kongano hilo litasaidia makundi mbali mbali kupata ajira pamoja na kudhibiti changamoto ya taka kuzagaa katika maeneo ya mkoa wa Manyara.

sauti ya kaimu katibu tawala idara ya huduma za uchumi na uzalishaji  mkoa wa manyara Faraja Ngelegeza

Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi wa kituo cha uhawilishaji na uendelezaji Technolojia(CDTT)-COSTECH Dr Norah Mdee amesema COSTECH ilibaini fursa zitokanazo na taka za majumbani ambapo tathimini ilionyesha teknolojia ya nzi chuma kuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti mazingira na kutengeneza bidhaa zenye tija katika jamii.

Sauti ya mwakilishi wa mkurugenzi wa kituo cha uhawilishaji na uendelezaji Technolojia(CDTT)-COSTECH Dr Norah Mdee

Nae mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) Dr Amos Nungu, amesema taka zinazooza zinaweza kubadilishwa kuwa bidhaa za thamani ikiwemo chakula cha mifugo.

Sauti ya mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) Dr Amos Nungu
picha ya mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) Dr Amos Nungu

Aidha, mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shaaban Mpendu, amesema hii ni fursa katika mji wa Babati kutokana na uzalishwaji wa taka kwani halmashauri hiyo inazalisha tani 85 za taka kwa siku.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shaaban Mpendu
picha ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shaaban Mpendu