FM Manyara

Viongozi msiwe sehemu ya migogoro ya maeneo

5 August 2026, 10:35 pm

Picha ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Remideus Mwema akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Halmashauri ya mji wa Babati

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati  mkoani Manyara Remideus Mwema amewataka Viongozi wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Babati kutokuwa sehemu ya migogoro ya maeneo yao ya kiutawala badala yake wawe wasuluhishi wa migogoro hiyo.

Na George Augustino

Kauli hiyo ameitoa leo katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Babati kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo ukiongozwa na mwenyekiti wake Yona Wawo, amesema migogoro isipotatuliwa huchangia kuwakwamisha Wawekezaji  kuwekeza katika maeneo hayo.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati

Kwa upande wake Meneja ufundi kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Babati (BAWASA) Sebastian Honolath akijibu swali la diwani wa kata ya maisaka  Abrahaman Kololi aliyetaka kujua ni kwanini wananchi wa eneo la Msasani wamekatiwa huduma ya maji na umeme, amesema serikali imetoa agizo hilo kutokana na umuhimu wa  mradi wa maji na usafi wa mazingira unaotarajiwa  kutekelezwa katika eneo hilo ambapo wananchi hao wamekataa kupewa fidia zao za maeneo.

Sauti ya Meneja ufundi wa BAWASA