FM Manyara
FM Manyara
21 September 2026, 5:17 pm

wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapobaini uwepo wa mtu anayeishi nchini bila kufuata taratibu za kisheria.
Na Emmy Peter
Idara ya Uhamiaji mkoani Manyara imewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kumjua jirani yake na kutoa taarifa kwa mamlaka pale wanapobaini uwepo wa mtu anayeishi nchini bila kufuata taratibu za kisheria.
Wito huo umetolewa Leo na inspector wa uhamiaji Awadh kilo ambae ni afisa wa Uhamiaji Mkoani hapaa wakati akitoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu na ushirikiano kati ya jamii na vyombo vya dola katika kudhibiti uhamiaji usio halali na kulinda usalama wa nchi.
Amesema kumjua jirani hakumaanishi kuwabagua watu kwa misingi ya utaifa, bali ni kuwa na uelewa wa watu wanaoishi katika jamii na kuhakikisha wageni wanafuata taratibu za kisheria za kuishi nchini.
Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapokuwa na taarifa au mashaka yanayohusiana na uhamiaji usio halali.