FM Manyara

Wananchi Babati wahimizwa kupima afya zao

11 November 2026, 11:58 am

Picha ya wataalam wa afya kutoka hospital ya mji wa Babati

Wananchi Wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kwenye wiki ya maadhimisho ya magonjwa yasioambukiza kwenye hospital ya mji Mrara ambayo imeanza November 9 hadi 14 mwaka huu.

Na Marino Kawishe

Akizungumza na Fm Manyara Radio kwenye kipindi cha mseto wa Leo Mratibu  wa magonjwa yasioambukiza Ngowi Restitute amesema dunia nzima huadhimisha wiki ya magonjwa yasioambukiza baada yakubaini ongezeko la magonjwa mbali mbali yanayohitaji Wananchi kupata elimu.

Sauti ya Mratibu wa magonjwa yasioambukiza Ngowi Restitute

Kwa upande wake Daktari Emanuel Mkonyi kutoka hospital ya mji mrara amefafanua magonjwa hayo na jinsi yakukabiliana nayo bila gharama kubwa ambazo zinaweza kupelekea kuyumba kiuchumi. 

Sauti ya Daktari Emanuel Mkonyi kutoka hospital ya mji mrara

Wiki ya magonjwa yasiyoambukiza huadhimishwa kila mwaka na kwa mwaka huu wa 2026 inaongozwa na kauli mbiu inayosema fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku mara tano kwa wiki ili kujikinga na magonjwa yasioambukiza kama shinikizo la juu la  damu, kisukari, saratani nk. Kila hatua  ni afya, kila jasho ni kinga.”