FM Manyara

Wazee Manyara waliopigana vita ya Uganda waiomba serikali iwalipe fidia

19 November 2026, 6:12 pm

Picha ya baadhi ya wazee Manyara

Wazee wanaoishi katika Kata ya Bashnet, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara, walioshiriki vita vya Uganda dhidi ya utawala wa Idd Amin mwaka 1978 hadi 1979, wameiomba Serikali kuwakumbuka na kuwalipa kifuta jasho kutokana na mchango wao katika kulinda na kujenga Taifa.

Na Mzidalfa Zaid

Wakizungumza wilayani Babati, wazee hao wakiongozwa na Daudi Panga, wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha, ikiwemo ukosefu wa uhakika wa huduma za matibabu, licha ya kuahidiwa kupewa vyeti maalumu vitakavyowawezesha kupata matibabu bure.

Sauti ya Wazee

Wazee hao wameiomba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutekeleza ahadi ya kuwalipa kifuta jasho na kuwapatia stahiki zao, wakieleza kuwa kwa sasa wamezeeka na wanahitaji msaada wa Serikali ili kuishi maisha yenye nafuu.