FM Manyara

Wizara ya Katiba na Sheria kutoa mafunzo ya uraia na utawala bora Manyara

23 October 2026, 5:10 pm

Picha ya Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Katiba katika Idara ya Katiba na Ufuatiliaji wa haki Wizara ya Katiba na Sheria Prosper Kisinini (kushoto) na Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Julieth Teemba (kulia)

Wizara ya Katiba na Sheria, kupitia Idara ya Katiba na Ufuatiliaji wa Haki, inatarajia kutoa mafunzo ya uraia na utawala bora kwa kamati za usalama za mkoa na wilaya, menejimenti za halmashauri zote, watendaji wa kata na vijiji pamoja na maafisa tarafa zote mkoani Manyara.

Na Mzidalfa Zaid

Kamati za usalama za mkoa na wilaya, menejimenti za halmashauri zote, watendaji wa kata na vijiji pamoja na maafisa tarafa zote mkoani Manyara wametakiwa kushiriki katika mafunzo ya uraia na utawala bora yanayotarajiwa kutolewa na wizara ya katiba na Sheria.

Akizungumza na FM Manyara, Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Katiba katika Idara ya Katiba na Ufuatiliaji wa haki Wizara ya Katiba na Sheria Prosper Kisinini amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha viongozi wajibu wao katika kusimamia ustawi wa wananchi na kuboresha utoaji wa huduma za serikali.

Picha ya Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Katiba katika Idara ya Katiba na Ufuatiliaji wa haki Wizara ya Katiba na Sheria Prosper Kisinini

Amesema mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza kutolewa Oktoba 26 mwaka huu, huku halmashauri zote za mkoa wa Manyara zikitarajiwa kufikiwa kwani mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha utendaji wa viongozi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Julieth Teemba, amesema wizara hiyo pia ina kituo cha huduma kwa wateja kinachowawezesha wananchi kupiga simu na kuwasilisha malalamiko yao ili kupata msaada wa kisheria kupitia namba ya simu ya bure 0800004004.

Sauti ya Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Julieth Teemba