FM Manyara

RC Shigela awataka wakuu wa wilaya kuimarisha ulinzi na usalama

5 October 2026, 9:58 pm

Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Martin Shigela akiwaapisha baadhi ya viongozi walioteuliwa hivi karibuni

Viongozi walioteuliwa hivi karibuni mkoani Manyara wameapishwa Leo mbele ya mkuu wa mkoa wa Manyara Martin Shigela, ambapo amewataka kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.

Na Mzidalfa Zaid

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, amewataka viongozi mkoani Manyara kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao huku  akiwataka wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Manyara kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa.

Shigela ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya kuwaapisha viongozi walioteuliwa hivi karibuni, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mkuu wa Wilaya ya Hanang , katibu tawala pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri, ambapo amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa viongozi hao wapya.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Martine Shigela
Baadhi ya viongozi walioapishwa Leo

Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Manyara, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema, amesema wataendelea kuwatumikia wananchi katika sekta mbalimbali kwa kuzingatia majukumu waliyopewa.

Aidha, katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño ambazo zimetabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Picha ya baadhi ya washiriki