FM Manyara
FM Manyara
13 October 2026, 8:08 pm

Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Manyara limeendelea kutoa huduma pamoja na elimu kwa wananchi na kufanya marekebisho ya miundombinu yake katika maeneo yote ya mkoa huo ili kukabiliana na madhara ya mvua za elnino zinazotarajiwa kunyesha
Na George Augustino
Shirika laumeme Tanzania Tanesco mkoa wa manyara limewataka Wananchi wa mkoa huo kufuata utaratibu pindi wanapohitaji huduma ya kuunganishiwa umeme na kuepuka kuwatumia mafundi ambao hawatambuliki maarufu kama vishoka .
Wito huo umetolewa na Mhandisi wa Tanesco mkoa wa manyara Regina Mvungi alipozungumza na fm manyara amesema Tanesco kwa sasa wanatumia mfumo rafiki wa kidigitali katika kuwahudumia wateja wake ambapo mteja akiufuata atapatiwa huduma kwa haraka na wepisi pia Tanesco kupitia Serikali ya Tanzania wameingia ubia na Benki ya CRDB wananchi wanaweza kukopeshwa fedha kwaajili ya kuunganishiwa umeme .
Aidha Regina amesema katika wiki ya huduma kwa wateja wameweza kukutana na wateja wao wakubwa wa viwanada na kuwapi mipango ya shirika pia wameweza kuwafikia wananchi katika wilaya zote za mkoa wa manyara na kuwapa elimu na kuendelea kuboresha miundombinu kwa kuondoa nguzo chakavu ili kukabiliana na madhara ya mvua za enino zinazotarajiwa kunyesha hapa nchini.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano kwa umma wa Tanesco mkoa wa Manyara Samweli Mandare amesema oparesheni ya kukagua na kuwabaini wanaohujumu miondombinu ya Shirika hilo ni endelevu na amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Shirika hilo kwa kuwafichua wote wanaohujumu miondombinu ya Shitika hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.