FM Manyara

Babati TC yaipongeza Deira School kwa kuongoza ufaulu 2025

18 April 2026, 5:39 pm

Picha ya mgeni rasmi akikabidhi kombe la ushindi kwa Deira English medium school

Deira English Medium School iliyopo wilayani Babati mkoani Manyara, imeibuka tena kidedea kwa kubeba makombe mawili ya ufaulu wa mitihani kwa kuongoza kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya Darasa la nne na darasa la Saba 2025.

Na Mzidalfa Zaid

Wamekabidhiwa makombe hayo pamoja na zawadi mbalimbali baada ya Halmashauri ya Mji Babati mkoani Manyara kutoa motisha maalum kwa shule ambazo zimefanya vizuri.

Kukabidhiwa kwa makombe hayo katika shule ya Deira English Medium School ni mwendelezo wa jitihada za muda mrefu, kwani shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri na kupata makombe kila mwaka na hali hiyo imeifanya shule hiyo kujijengea heshima kubwa ndani na nje ya Mkoa wa Manyara.

Meneja wa shule ya English medium school Gaspar Silvery amesema Shule hiyo imefanikiwa kutwaa makombe mawili muhimu, jambo linaloonyesha ubora wa hali ya juu katika ufundishaji na malezi ya wanafunzi wake.

sauti ya Meneja wa shule ya English medium school Gaspar Silvery

Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa ni Kaim afisa elimu mkoa wa Manyara ambae ni afisa elimu taaluma mkoa wa Manyara Allan Said , amezipongeza shule ambazo zimefanya vizuri ikiwemo shule hiyo ya Deira English medium school kwani kwa kukuza kiwango Cha elimu katika mkoa wa Manyara.

sauti ya Kaim afisa elimu mkoa wa Manyara ambae ni afisa elimu taaluma mkoa wa Manyara Allan Said

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Babati, CPA Shaaban Mpendu ameupongeza uongozi na walimu wa Deira English Medium School kwa kazi kubwa wanayoifanya, amesema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya nidhamu, ubunifu wa walimu pamoja na usimamizi madhubuti wa taaluma.

sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Babati, CPA Shaaban Mpendu

Nae mkuu wa shule ya Deira English medium school mkuu wa shule Bosco Godfrey amewaomba wazazi wanahitaji kujiunga na shule hiyo wawapeleke watoto wao ili wapate elimu iliyobora kwa gharama nafuu.

sauti ya mkuu wa shule ya Deira English medium school
picha ya baadhi ya walimu wa shule ya Deira wakisherehekea ushindi
picha ya msafara wa maandamano ya amani kusherehekea kombe la ushindi wa shule ya Deira