FM Manyara

So They Can yakabidhi miradi ya shilingi Millioni 267 Babati Dc

3 July 2026, 7:15 pm

Picha ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daniel Sillo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gedemara kilichopo Wilayani Babati mkoani Manyara

Na Marino Kawishe

Shirika la So They Can Tanzania  limekabidhi miradi miwili ambayo ni  bweni la wasichana na nyumba Tatu za waalimu zenye thaman ya zaidi ya shilingi milion 265, kwa halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara ambayo imekamilika kwa asilimia mia moja.

Akizungumzia miradi hiyo mbele ya mgeni Rasmi Naibu Spika Daniel Sillo, Meneja mkazi wa shirika hilo Roselyne Mariki amesema kukamilika kwake ni utekelezaji wa mpango wa shirika hilo kwenye kuboresha miundo mbinu ya sekta ya elimu ambayo inatekelezwa katika kata nne za halmashauri ya wilaya ya Babati na ambayo inaungwa mkono na wananchi wa maeneo hayo.

Sauti ya Meneja mkazi wa shirika la So They Can

Kwa upande wa Mgeni Rasmi Kwenye Halfa hiyo Naibu Spika Wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daniel Baran Sillo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji na kuvutia mashirika binafsi kufanya shughuli zao hapa Nchini. 

Sauti ya Naibu Spika Wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa upande wao wanafunzi pamoja na mwalimu wa shule ya msingi Manyara inayopakana na hifadhi ya Tarangire wametoa pongezi zao kwa shirika la So They Can Tanzania kwa kuwawezesha kupata nyumba za waalimu. 

Aidha kukamilika kwa mradi huo kutawawezesha wanafunzi wanaokaa mbali hasa wa kike kufanya vizuri katik masomo yao na kuondokana na changamoto za vishawishi vinavyopelekea kupata ujauzito na kusitisha masomo yao.

Sauti ya mwalimu na wanafunzi