FM Manyara
FM Manyara
29 July 2026, 6:44 pm

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, George Mhina, amewahimiza wananchi na wawekezaji kutumia fursa zilizopo kwa kuanzisha vituo vya mafuta katika maeneo ya vijijini ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
Na Mzidalfa Zaid
Mhina amesema kuwa uwekezaji katika vituo vya mafuta vijijini utarahisisha upatikanaji wa nishati, kuchochea shughuli za kiuchumi na kufungua fursa za ajira katika maeneo husika.
Aidha, amesisitiza kuwa wawekezaji wanapaswa kufuata taratibu na kanuni zinazowekwa na EWURA ili kuhakikisha vituo vinajengwa na kuendeshwa kwa kuzingatia viwango vya usalama na ubora wa huduma.