FM Manyara
FM Manyara
18 September 2026, 11:39 pm

Mkoa wa Manyara umeanza kuchukua hatua za kukabiiliana na athari za mvua za elinino katika maeneo ambayo yanahisiwa kuathiriwa na mvua hizo.
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martine Shigela, amefanya ziara ya kutembelea maeneo ya makazi ya wananchi yanayopakana na Ziwa Manyara, ambayo yanaweza kuathiriwa na mvua za El Niño, kwa lengo la kuchukua tahadhari za
awali.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Magara, Shigela amewaagiza viongozi wa TANROADS, TARURA pamoja na wataalamu mbalimbali kuchukua hatua za haraka, ikiwemo kuelekeza maji katika maeneo yasiyo na makazi ya wananchi, ili kupunguza uwezekano wa madhara yatokanayo na mvua hizo.
Amewataka wananchi mkoani Manyara kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño, ikiwemo kuondoka katika maeneo ya mabondeni na maeneo mengine yanayoweza kuwa hatarini wakati wa mvua kubwa.

Kwa upande wake afisa mazingira mkoa wa Manyara Michael Gwandu amesema wanaendelea kuchukua hatua kwa maeneo yenye hatari ya kukumbwa na mafuriko kuhakikisha wanachukua tahadhari za haraka.
Awali Diwani wa kata ya Magara ameiomba serikali kuhamisha mkondo wa maji kwenye makazi ya watu ili wananchi wasipate madhara zitakaponyesha mvua za Elinino.
