FM Manyara

Askari wa uhifadhi waaswa kuendelea kulinda rasilimali za Taifa.

31 July 2026, 7:40 pm

Picha ya Kamishna msaidizi wa uhifadhi anayesimamia ulinzi kwa Kanda ya Kaskazini Rajabu Hochi

Tanzania imeungana na Mataifa mengine Dunia Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Askari wa uhifadhi maarufu kama Rangers Day.

Na Marino Kawishe

Akisoma Risala ya siku ya Rangers  Afisa wanyamapori kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Babati Beatrice Onesmo mbele ya mgeni Rasmi Kamishna  msaidizi wa uhifadhi  Rajabu Shabani Hochi anayesimamia Ulinzi kwa Kanda ya Kaskazini amesema siku hii imetengwa maalumu ili kuenzi mchango wa Askari wa uhifadhi waliojitolea maisha yao kulinda rasilimali za nchi.

Sauti ya Afisa wanyama Pori kutoka halmashauri ya Wilaya ya Babati

Akizungumza mbele ya Askari wa uhifadhi kutoka taasisi ya TANAPA, TAWA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jamii ya Burunge (Burunge WMA) Kamishna msaidizi wa uhifadhi anayesimamia ulinzi kwa Kanda ya Kaskazini amesema Askari wa uhifadhi  si walinzi pekee wa uhifadhi bali hata Rasilimali nyingine za nchi.

Sauti ya Kamishna msaidizi wa uhifadhi anayesimamia ulinzi kwa Kanda ya Kaskazini

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi  ya Chem Chem Festo Mangalia amesema Taasisi hiyo itaendelea kufanya uhifadhi wa pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo TANAPA, TAWA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jamii ya Burunge (Burunge WMA) ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo mbali mbali kwa Askari ili kukabilian kikamilifu na majangili wanaovamia ecologia ya Tarangire-Manyara  huku wakiwa na mpango wa kushirikisha jamii elimu ya uhifadhi hadi kwenye shule za msingi na sekondari. 

Sauti ya Festo Mangalia

Siku ya Kimataifa ya Askari wa uhifadhi maarufu kama World Rangers Day huadhimishwa kila ifikapo julai 31 ya kila mwaka na kaulimbiu kwa mwaka huu ni “Rangers are Gurdians of the Changing Planet”