FM Manyara
FM Manyara
12 June 2026, 7:26 pm

Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP kwa kushirikiana na baadhi ya wakulima kutoka vituo vya taarifa na maarifa vya mamire na Murray mkoani Manyara wamefanya mafunzo ya pamoja ya nadharia na vitendo yanayohusu Kilimomisitu.
Akizungumza na Fm Manyara Msimamizi wa mafunzo hayo ya siku nne yaliyofanyika katika kijiji cha Mamire Wilayani Babati Kutoka TGNP Ester William amesema lengo la semina hiyo kwa wakulima hao ni kujifunza dhana ya Kilimo misitu na kanuni za kilimo Ikolojia pamoja na masuala ya Jinsia na kilimo himilivu kwa mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake mtaalamu wa Kilimomisitu anayefanya kazi na mtandao huo na mtoa mada kwenye mafunzo hayo Valence Kiangi ameeleza sababu zinazopelekea kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha afisa kilimo wa kata ya mamire Emanuel Lohaay Amebainisha faida zakufanya Kilimomisitu kwa wananchi huku akigusia kilimo hicho kama kitu ambacho kikitiliwa mkazo kinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Nao baadhi ya washiriki katika semina hiyo ya Kilimomisitu wamekiri hawakuwahi kupatiwa mafunzo kama hayo hapo awali na kutoa pongezi kwa mtandao wa Jinsia Tanzania kwa kuona fursa hiyo kwa vituo hivyo vya taarifa na maarifa.
Mafunzo ya Kilimomisitu yamefanyika kwa nadharia na vitendo huku wakulima walioshiriki wakipata nafasi yakutengeneza mbolea ya asili iitwayo Bokashi ambayo hutengenezwa bila kemikali kwa kutumia rasilimali zinazopatikana kwenye maeneo ya wakulima wanaofanya kilimo cha kutumia mbegu za asili.
