FM Manyara
FM Manyara
6 August 2026, 12:36 am

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeendelea kutoa elimu kwa Wakulima na Wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia Bima za kilimo pamoja na Bima za Afya ili kujikinga na hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na majanga mbalimbali.
Na Emmy Peter
Kauli hiyo imetolewa na Afisa kutoka Tira, Goodluck Masawa, katika viwanja vya maonesho ya nanenane Temi Njiro Mkoani Arusha, ambapo amewahimiza Wakulima kutumia Bima za kilimo kama njia ya kulinda uwekezaji wao na kuhakikisha wanaendelea na uzalishaji hata wanapokumbwa na changamoto ya ukame mashambani.
Kwa upande wao, Wanafunzi waliotembelea banda la Tira wamepewa elimu kuhusu majukumu ya Taasisi hiyo pamoja na umuhimu wa bima katika maisha ya kila siku, hatua inayolenga kujenga uelewa wa bima kwa kizazi cha sasa nachabaadae.
