FM Manyara
FM Manyara
3 October 2026, 8:28 am

Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kutumia Fursa ya Kliniki ya ardhi kumiliki ardhi kikamilifu.
Na Mzidalfa Zaid
Serikali imewataka wananchi kutumia fursa ya clinic ya ardhi inayoendelea Katika halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara kwa kupata elimu ya Umiliki wa ardhi na matumizi ya mfumo wa E- Ardhi, kupata Hati pamoja na Utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Rai hiyo imetolewa na CPA. Shaaban A. Mpendu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Babati wakati alipokuwa katika kliniki hiyo iliyoanza tarehe 22 Septemba hadi 3 Oktoba 2026 katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa yenye kauli mbiu “ARDHI KLINIKI KIDIJITALI,E-Ardhi:Huduma Popote”.
Aidha ameeleza kuwa kliniki hiyo imetatua changamoto za ardhi kwa kiwango kikubwa na kueleza kuwa Ofisi ya ardhi halmashauri ya mji Babati ipo tayari kwa kuwahudumia wananchi kwa kuwasikiliza katika masuala yahusuyo kero za ardhi.
Naye Erick Peter Makundi Kamishina msaidizi wa Ardhi mkoa Manyara ameeleza kuwa jumla ya Hati 250 zimetolewa katika klininik hiyo ikiwa malengo ni kufikia idadi ya 750 hadi kutamatika kwa zoezi hilo .
Huduma zinazotolewa katika Kliniki hiyo ni pamoja na elimu ya umiliki wa ardhi na matumizi ya mfumo wa E- Ardhi, Utoaji wa hati, utatuzi wa migogoro ya ardhi pamoja na ile inayohusu mirathi utoaji wa ankara za malipo ya Kodi pamoja na usajili wa nyaraka mbalimbali.