FM Manyara

Maonyesho ya Tanzanite Manyara trade fair yaendelea kupamba moto

16 October 2026, 10:19 pm

Picha ya baadhi ya mabanda katika maonyesho ya Tanzanite Manyara trade fair

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair yanayoendelea katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa, Babati, ili kujionea bidhaa na fursa mbalimbali za kibiashara.

Na Mzidalfa Zaid

Maonyesho ya Manyara Tanzanite trade fair yanaendelea katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa,ambapo Taasisi na wafanyabiashara mbalimbali kutoka mikoa tofauti wameshiriki .

Meneja wa Chemba ya Taifa ya Biashara mkoani Manyara, Lerunde Laizer, amesema wafanyabiashara na taasisi mbalimbali zinazoendelea kushiriki katika maonyesho hayo zinatoa elimu kwa wananchi pamoja na kuonyesha na kuuza bidhaa mbalimbali.

Aidha, amewataka wafanyabiashara wanaohitaji kushiriki katika maonyesho hayo kutumia fursa hiyo kutangaza biashara zao, kuongeza wateja na kupanua wigo wa masoko yao.

Sauti ya Meneja wa Chemba ya Taifa ya Biashara mkoani Manyara, Lerunde Laizer

Amesema maonyesho hayo ni sehemu muhimu ya kuwaunganisha wafanyabiashara na wateja, kujenga mahusiano ya kibiashara na kuwapa washiriki nafasi ya kujitangaza, huku akihimiza wananchi kutumia maonyesho hayo kujifunza na kufahamu bidhaa na huduma zinazopatikana kutoka kwa wafanyabiashara na taasisi mbalimbali.