FM Manyara
FM Manyara
14 October 2026, 10:19 am

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) mkoa wa Manyara imesema katika siku kumi zijazo, mkoa huo unatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua katika baadhi ya maeneo.
Na Mzidalfa Zaid
Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) mkoa wa Manyara, Salma Amour, amesema hali hiyo imejitokeza kuanzia October 11 Hadi October 20.
Amour amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalamu wa hali ya hewa kutokana na utabiri wa mvua za El Niño, ili kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
Aidha Amewahimiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa ajili ya kupata mwelekeo wa hali ya hewa na kuchukua hatua stahiki katika shughuli zao za kila siku.