FM Manyara
FM Manyara
19 October 2026, 11:46 pm

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutumia kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka kutembelea Mlima Hanang na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika mlima huo.
Na Mzidalfa Zaid
Katika kipindi hiki Cha Kuelekea mwisho wa mwaka , wananachi mkoani Manyara wametakiwa kutumia fursa hiyo kutalii ndani ya hifadhi asilia ya mlima hanang
Wito huo umetolewa na Afisa Utalii kutoka Hifadhi Asilia ya Mlima Hanang, Gasper Mwapinga, amesema hifadhi hiyo ina vivutio mbalimbali vinavyoweza kuwavutia watalii kutoka ndani na nje ya mkoa wa Manyara.
Mwapinga amesema baadhi ya vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ni pamoja na maporomoko ya maji, Mlima Hanang wenyewe pamoja na aina mbalimbali za ndege.