FM Manyara

TFRA, Crop Bioscience mguu sawa kuinua kilimo

20 October 2026, 5:27 pm

Picha ya Meneja wa TFRA Kanda ya kaskazini pamoja na mkulima

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kushirikiana na kampuni ya Crop Bioscience iliyopo Kijiji cha Kiongozi, Kata ya Marakea, Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara, zimeingia makubaliano ya kuanzisha shamba la mfano litakalotumika kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbolea na mbinu bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija.

Na Mzidalfa Zaid

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Meneja wa TFRA Kanda ya Kaskazini Gothard Liampawe, alipotembelea shamba la kampuni hiyo linaloongozwa na Mkurugenzi wake, Wilfred Mushobozi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani inayofanyika Oktoba 13 kila mwaka.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Liampawe ameitaka kampuni ya Crop Bioscience kuendelea kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea katika shughuli za kilimo ili kuongeza uzalishaji na kupata mavuno yenye tija.

Sauti ya Meneja wa TFRA Kanda ya Kaskazini Gothard Liampawe,
Picha ya Meneja TFRA Kanda ya kaskazini pamoja na mkulima

Amesema kuanzishwa kwa shamba la mfano kutatoa fursa kwa wakulima kujifunza kwa vitendo kuhusu matumizi sahihi ya mbolea pamoja na mbinu bora za kilimo zitakazosaidia kuboresha uzalishaji wa mazao.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Wilfred Mushobozi amesema Kampuni ya Crop Bioscience inajishughulisha na uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali, yakiwemo mahindi, choroko, maharage na migomba.

Sauti ya mkulima