FM Manyara

Naibu waziri wa maji atoa maagizo kukamilisha miradi ya maji Manyara

6 October 2026, 10:32 pm

Picha ya naibu waziri wa maji Kundo Methew

Naibu waziri wa maji Kundo Methew ameziagiza Mamalaka za maji mkoani Manyara kuhakikisha wanakamilisha miradi ya maji ambayo Iko hatua za mwisho kukamilika kabla hawajaanzisha miradi mipya.

Na Mzidalfa Zaid

Naibu waziri wa maji Kundo Methew ameanza zaiara yake mkoani Manyara ambapo ametoa maagizo kwa viongozi wa mamlaka kukamilisha miradi iliyobakiza asilimia chache kukamilika.

Ametoa maelekezo hayo Leo katika ziara yake ya kikazi ambayo ameianza Leo mkoani Manyara amesema ni muhimu fedha zinazotolewa zikamilishe miradi ambayo imebakiza asilimia chache  kukamilika ili wananchi waanze kunufaika na miradi hiyo.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuandaa vyombo vya kuvuna maji ya mvua katika kuchukua tahadhari endapo miundombinu ya maji itaathiriwa na mvua za elinino.

Sauti ya Naibu waziri wa maji Kundo Methew

Kwa upande wake meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mkoa wa Manyara injinia James kionaumela amesema upatikanaji wa maji katika mkoa wa Manyara kwa maeneo ya mjini ni asilimia 98 na kwa vijijini ni asilimia 84.

Sauti ya meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mkoa wa Manyara injinia James kionaumela

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Babati ,katibu tawala wilaya ya Babati Thobias Abwaro amemuomba  Naibu waziri wa maji kuaanda sehemu maalumu ya kuhifadhia maji taka kutokana na mji wa Babati kuendelea kukua.

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Babati Thobias Abwaro
Picha ya naibu waziri wa maji Kundo methew akikagua mradi wa maji Ayasanda
Chanzo Cha maji ambacho kimetembelewa na naibu waziri wa maji