FM Manyara
FM Manyara
17 October 2026, 10:27 pm

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeziagiza benki zote za biashara mkoani Manyara kuanzia leo kupokea fedha zilizochakaa na ambazo hazifai tena kuendelea kutumika katika mzunguko wa fedha.
Bank za biashara mkoani Manyara zimeagizwa kuhakikisha zinapokew fedha zilizochakaa, kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wakilalamikia fedha zilizochakaa kukataliwa katika baadhi ya bank za biashara.
Agizo hilo limetolewa leo na Meneja wa Uendeshaji wa Benki Kuu ya Tanzania, Ofisi ya Arusha, Cletus Mwakalinga, wakati akizungumza katika Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair yanayoendelea katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa, mkoani Manyara.
Mwakalinga amesema ili fedha zilizochakaa ziweze kupokelewa, zinapaswa kuwa halali, kuwa nzima kwa angalau asilimia 75 ya sehemu yake ya awali, na zisiwe zimeharibiwa kwa makusudi.

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kutunza fedha zao katika mazingira bora ili kuzuia zisiharibike mapema, akisisitiza umuhimu wa kuepuka kuzihifadhi katika sehemu zisizofaa ambazo zinaweza kusababisha kuchakaa au kuharibika kwa fedha hizo.