FM Manyara

TRA Manyara yahimiza wafanyabiashara kujisajili ndani ya siku 14

30 September 2026, 10:18 pm

Picha ya afisa wa Kodi wa TRA Manyara

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Manyara imewataka wananchi kuhakikisha ndani ya siku 14 wanajisajili katika mfumo tangu kuanza biashara.

Na Emmy Peter

Wananchi na walipa kodi mkoani Manyara wamehimizwa kuhakikisha kuwa ndani ya siku 14 tangu kuanza biashara, wanafika katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kujisajili katika mfumo wa mamlaka hiyo.

Afisa wa Kodi wa TRA mkoani Manyara Faraja Juma Mtani amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha wafanyabiashara wanatimiza wajibu wao wa kisheria na kushiriki katika kuchangia pato la taifa.

Sauti ya Afisa wa Kodi wa TRA mkoani Manyara Faraja Juma

Kwa upande wake, Afisa Mahusiano wa TRA, Justin Aloyce, amesema mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimu kuhusu maadili kwa watumishi pamoja na wateja, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma na kujenga mahusiano mazuri kati ya TRA na wananchi.

Sauti ya Afisa Mahusiano wa TRA, Justin Aloyce
Picha ya afisa kodi wa TRA mkoa wa Manyara akifanya kipindi ndani ya studio za Fm Manyara radio