FM Manyara
FM Manyara
4 June 2026, 4:08 pm

Chama kikuu Cha ushirika mkoa wa Manyara (RIVACU)kimefanya mkutano mkuu wa mwaka ambapo mipango mbalimbali imewasilishwa ikiwemo miradi itakayoendelezwa pamoja na uzalishaji kwa ajili ya kukuza chama hicho.
Na Mzidalfa Zaid
Akiongea baada ya kikao hicho mwenyekiti wa bodi ya chama kikuu Cha ushirika mkoa wa Manyara (RIVACU)Yuda Sulle amesema miradi hiyo ni pamoja uendelezaji wa viwanja vya chama kikuu, utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi za ghala pamoja na mradi wa mashine ya kukamua alizeti.
Kwa upande wake meneja wa chama kikuu Cha ushirika mkoa wa Manyara (RIVACU)Pendoeli Valentine amesema wanatarajia kuanzisha saccos ya chama kikuu itakayosaidia kupata pembejeo nyingi na kuwasaidia wakulima ambao ni wanachama.

Nae mrajis msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Manyara Absalom Cheliga ,amesema Lengo la kikao hicho ni kufanya tathimini ya maazimio ya kikao kilochopita pamoja na kuweka mipango mikakati.
Aidha, baadhi ya washiriki wa kikao hicho wamesema mwaka uliopita walikumbana na changamoto ya mazao kushuka bei, huku wakifurahishwa na uwekezaji unatarajiwa kuwekezwa ndani ya chama .
