FM Manyara

Wataalam: Ugonjwa wa sikoseli si laana

21 April 2026, 7:05 pm

Picha ya baadhi ya madaktari wakitoa elimu ya ugonjwa wa sikoseli kwa waandishi wa habari.

 Jamii mkoani Manyara imetakiwa kuachana na imani potofu kuwa ugonjwa wa sikoseli unasababishwa kwa kulogwa au laana, bali ugonjwa huo unasababishwa na kurithi.

Na Mzidalfa Zaid

Hayo yameelezwa na mratibu wa sikoseli na Hemofilia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Astera Mpoto wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Manyara kuhusu ugonjwa wa sikoseli na Hemofilia, ambapo amewataka waandishi wa habari kuelimisha jamii kuwa magonjwa hayo yanatokana kwa kurithi.

Sauti ya mratibu wa sikoseli na hemofilia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Astera Mpoto

Kwa upande wake dokta bingwa wa watoto kutoka hospital ya rufaa ya mkoa wa Manyara dokta Joshua Girlabayda amesema katika mkoa wa Manyara watoto wenye ugonjwa wa sikoseli linazidi kuongezeka mwaka Hadi mwaka ambapo amesema katika hospital ya mkoa wa Manyara wanatibu watoto wenye tatizo hilo katika clinic za watoto.

Sauti ya daktari bingwa wa watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Joshua Girlabayda

Naye daktari bingwa wa magonjwa ya damu kutoka hospital ya Kanda ya Benjamin Mkapa Stella Malangahe, amesema wameanzisha huduma ya upandikizaji  uloto kwa watoto wenye changamoto ya sikoseli ili kuisaidia kutoa matibabu sahihi ambapo mpaka Sasa watoto 30 wamepatiwa huduma hiyo.

Sauti ya daktari bingwa wa magonjwa ya damu kutoka Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa Stella Malangahe

Nao baadhi ya waandishi wa habari akiwemo afisa habari mkoa wa Manyara Ruth Kyelula wamesema elimu ambayo wameipata wataifikisha kwa jamii ili kupata kuelewa kuhusu. ugonjwa huo.

Sauti ya baadhi ya waandishi wa habari akiwemo afisa habari mkoa wa Manyara Ruth kyelula
Baadhi ya waandishi wa habari