Mazingira FM

Wazazi CCM Bunda kukutana kutathmini uchaguzi serikali za mitaa kupitia baraza

30 December 2024, 6:40 pm

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Bunda Ndugu wakili Leonard Magwayega

Jumuiya ya wazazi ni kama imesahaulika hivi wakati mwingine tunatoa pesa zetu mfukoni ili kufanya kazi za jumuiya tunataka kuwa na mradi utakaowezesha kuacha kuwa ombaomba” Magwayega “

Na Adelinus Banenwa

Jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Bunda kufanya kikao kutadhmini uchaguzi wa serikali za mitaa wa Nov 27, 2024 wilayani Bunda.

Akizungumza na radio Mazingira Fm mwenyekiti wa jumuiya hiyo Ndugu wakili Leonard Magwayega amesema kikao hicho cha tathmini kitafanyika tarehe 31 Dec 2024 ambapo lengo kuu ni kujadili matokeo ya uchaguzi na mipango kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025

Sauti ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Bunda Ndugu wakili Leonard Magwayega

Miongoni mwa mambo mengine pia wajumbe watakuwa na nafasi ya kujadili miradi mbalimbali itakayoisaidia jumuiya hiyo kuepukana kuwa ombaomba.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Bunda Ndugu wakili Leonard Magwayega

Pia amesema miongoni mwa jumuiya zilizosahaurika ndani ya chama cha mapinduzi ni pamoja na jumuiya ya wazazi ambapo haina wabunge  wala  diwani ukilinganisha na jumuiya zingine, hivyo ni vema kukawepo mradi utakaowasaidia kiuchumi kutokana na mara nyingi kuwategemea wadau kiuendesha shughuli zao wakiwemo wabunge ambao wakati mwingine wanachoka kutoa msaada huo.

Sauti ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Bunda Ndugu wakili Leonard Magwayega