Mazingira FM

UVCCM Bunda yawakumbusha wabunge, madiwani kutoisahau jumuiya hiyo

14 December 2024, 8:39 pm

Wajumbe wa Baraza la Vijana chama cha mapinduzi Bunda UVCCM

Kilio kukubwa cha vijana hao ni kutaka ushirikiano kutoka kwa viongozi hao ikiwa ni pamoja na madiwani na wabunge.

Na Adelinus Banenwa

Umoja wa vijana chama cha mapinduzi wilayani Bunda wamewasihi viongozi waliochaguliwa kupitia chama hicho kutoisahau jumuiya hiyo kutokana na majukumu makubwa iliyonayo kwa chama hicho.

Vijana  wameyasema hayo katika baraza la kawaida la jumuiya ya Vijana wilaya ya Bunda ambalo limefanyika leo Dec 14, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine wamepata nafasi ya kutathmini  matokeo ya uchaguzi serikali za mitaa uliofanyika  tarehe 27 Nov 2024.

Katibu wa UVCCM Bunda Cde Pendo Machilu

Katika hoja zao vijana hao wamesema mara nyingi wamekuwa wakitumika sana kipindi cha uchaguzi lakini viongozi hao wakishaingia madarakani huisahau jumuiya hiyo ya vijana

Sauti ya wajumbe wa baraza la vijana UVCCM Bunda
Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Ndugu Muhammad Msafiri

Naye mwenyekiti wa jumuiya ya vijana chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Ndugu Muhammad Msafiri amesema umoja wa vijana una imani kubwa na viongozi walipo madarakani kutokana na kazi kubwa anayoifanya mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania lakini kilio kukubwa cha vijana hao ni kutaka ushirikiano kutoka kwa viongozi hao ikiwa ni pamoja na madiwani na wabunge.

Sauti ya Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Ndugu Muhammad Msafiri
Emmanuel Kija katibu wa Mbunge jimbo la Bunda mjini

Kwa upande wake Emmanuel Kija ambaye  katibu wa Mbunge jimbo la Bunda mjini  kwa niaba ya  mgeni Rasmi Mhe Robert Chacha Maboto ambaye ndiye Mbunge wa jimbo  amewahasa vijana kuzingatia nidhamu pia kutowasema vibaya viongozi waliopo kwa kuwa kufanya hivyo wanakuwa wanakisema vibaya chama ambacho ndicho kilichomuamini kiongozi huyo.

Aidha ndugu kija amewashauri vijana hao kuhakikisha wanamiliki  uchumi kutokana na kwamba wao ni nguvu kazi ya chama cha mapinduzi.

Sauti ya Emmanuel Kija katibu wa Mbunge jimbo la Bunda mjini