Wazazi, walezi washauriwa kuwakanya watoto wanapokosea
13 December 2024, 7:01 am
“Vimeanza kuwepo viashiria vya udokozi na wizi nyakati za mchana na usiku katika baadhi ya maeneo katika Mtaa wa Majengo pia watoto wameanza kupiga mafataki hali hiyo haikubaliki”
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi katika mtaa wa Majengo kata ya Kabarimu mjini Bunda kuwalinda watoto wao kujiepusha na masuala ya uharifu kuelekea kipindi hiki cha sikukuu za kufunga mwa 2024.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa mtaa huo ndugu Mawazo Mussa Ntonda alipozungumza na Mazingira Fm kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika mtaa wake kuelekea sikukuu za kufunga mwaka.
Mwenyekiti Mawazo amesema vimeanza kuwepo viashiria vya udokozi na wizi nyakati za mchana na usiku katika baadhi ya maeneo katika mtaa wa Majengo pia watoto wameanza kupiga mafataki hali hiyo haikubaliki na yeyote atakayebainika au kukamatwa eno la tukio yeye kama mwenyekiti wa mtaa hatoweza kumtetea