Waziri Gwajima: Tumieni lugha ya wazi kueleza madhara ya ukeketaji
10 December 2024, 10:30 am
Mwaka 2024 matukuo yaliyoripotiwa 1099 ukilinganisha na matukio 1163 sawa kupungua kwa matukio 64 ambayo ni sawa na asilimia 5.8
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa ukosefu wa sheria mahsusi inayopinga vitendo vya ukeketaji, ukosefu wa nyumba salama za serikali na upungufu wa ofisi za madawati ya jinsia kwenye vituo vya polisi bado ni changamoto katika kutokomeza ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji kwenye jamii.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizofanyika Nyamongo Tarime kamanda wa polisi kanda maalumu Tarime Rorya ACP Marck Njera amesema hatua kubwa imefanyika katika kutoa elimu kwa jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kutokomeza matukio ya ukatili kwenye jamii utokanao na mila na desturi ambapo matukio ya ukatili kwa mwaka huu 2024 yamepungua ukilinganisha na mwaka 2023.
ACP Marck amesema kwa mwaka 2024 matukuo yaliyoripotiwa 1099 ukilinganisha na matukio 1163 sawa kupungua kwa matukio 64 ambayo ni sawa na asilimia 5.8
Aidha kamanda Marck amesema matukio ya ukeketaji mwaka huu yameripotiwa zaidi kuliko miaka mingine kutokana na jamii kupata elimu juu ya madhara yatokanayo na ukatili.
Kwa upande wake waziri wa maendeleoya jamii jinsia na makundi maalum Mhe Doroth Gwajima amesema ni wakati sasa jamii kuzungumza mambo kwa uwazi hasa madhara ya mojakwamoja yatokanayo na ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji
Akitolea mfano ya madhara hayo ikiwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi inayopelekea wengine kupoteza maisha, makovuau ulemavu wa kudumu, changamoto ya bakteria kwenye mfumo wa uzazi na mkojo, changamoto wakati wa kujifungua hali ambayo hupelekea vifo vya mtoto au mama au wote kwa pamoja, changamoto ya kisaikolojia miongoni kwa madhara mengine.
Amesema katika msimu huu wa ukeketaji unaoendelea operesheni ya jeshi la polisi Tarime – Rorya iliyofanyika kuanzia Dec 3, 2024 jumla ya watoto 180 wamenusurika kwenye ukeketaji na kupelekwa kituo cha kupinga ukeketaji cha ATFGM Masanga.
Aidha mhe Doroth amesema kiwango cha ukeketaji kwa mkoa wa mara kimeshuka hadi kufikia asilimia 28 kilinganishwa na mikoa ya arusha na manyara yenye wastani wa asilimia 43, singida 20 dodoma asilimia 18 na tanga asilimia 9 ambapo takwimu zinaonesha kwa upande wa vijijini ukeketaji unaongezeka ukilinganishwa na mijini kutokana na elimu.