‘Hoja za wenye ulemavu zisikilizwe’
5 December 2024, 9:53 am
Katiba ya Tanzania imetoa uhuru wa watu kujieleza lakini changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu ni hoja zao na mawazo yao kutopewa nguvu katika jamii.
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa mapokeo hafifu ya hoja zinazotolewa na watu wenye ulemavu ni chanzo cha kuminya uhuru wa kujieleza kwa kundi hilo kwenye jamii.
Hayo yamesemwa na Juma Waryoba Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji wa Bunda alipozunzumza kupitia Radio Mazingira FM katika program ya Uhuru wa Kujieleza inayodhaminiwa na UTPC ambapo ndugu Waryoba amesema katiba ya Tanzania imetoa uhuru wa watu kujieleza lakini changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu ni hoja zao na mawazo yao kutopewa nguvu katika jamii.
Kwa upande wake Rebecca Gibore mwanaharakati na mhudumu wa afya ngazi ya jamii amesema jukumu kubwa jamii ililonalo ni kukubali kupokea elimu inayotolewa ambapo kwa sasa kwa upande wa wanawake mabadiliko yapo tofauti na upande wa watu wenye ulemavu