Mazingira FM

Madiwani Bunda Mjini watishia kwenda mahakamani kudai fidia Nyatwali

14 November 2024, 7:41 pm

Madiwani wanahitaji kujua thamani ya fedha kwa mali za halamshauri ya mji wa Bunda ambazo zimefanyiwa tathimini katika kata ya Nyatwali ambapo imechukuliwa na Tanapa.

N Adelinus Banenwa

Madiwani wa Halmashauri ya Bunda mji watishia kwenda mahakamani juu ya malipo ya fidia kwa mali za halmashauri katika eneo Nyatwali eneo ambalo limechukuliwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kama Mapitio ya Wanyama

Madiwani hao wamesema wanaona Kuna kificho juu yatathimini ya mali hizo na kusema kama hali itaendelea hivyo wataenda kudai haki hiyo hakamani.

Hayo yameelezwa na baadhi ya madiwani baada kuwasiliswa kwa hoja binafsi kutoka kwa Mh. Diwani Flavian Nyamageko Diwani wa kata ya Bunda stoo ambapo alihoji juu ya thamani ya fedha kwa mali za Serikali ambazo zimefanyiwa tathimini katika kata ya Nyatwali ambapo imechukuliwa na Tanapa.

Sauti ya madiwani

Akitoa ufafanuzi wa hoja hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Salimu Mtelela amesema kuwa mpaka Sasa hawajapata majibu ya kiasi gani na fidia hiyo inalipwaje ila ofisi ya mkuu wa wilaya inaendelea na mawasiliano na mamlaka za wizara ya fedha ili kupata majibu.

Sauti ya katibu tawala