Serengeti yashinda tena hifadhi bora Africa
22 October 2024, 2:12 pm
Hifadhi ya taifa ya Serengeti imeshinda kwa mara ya sita mfurulizo tuzo ya kuwa hifadhi bora barani afrika
Na Adelinus Banenwa
Hifadhi ya taifa ya Serengeti imeshinda kwa mara ya sita mfurulizo tuzo ya kuwa hifadhi bora barani afrika
Akizungumza na waandishi wa habari kamishna msaidizi mwandamizi wa uhifadhi Stephano Msumi ambaye ni mkuu wa hifadhi ya taifa ya Serengeti amesema ninfaraja kubwa kwa taifa kuona jitihada za kuitunza hifadhi ya Serengeti inakuwa na matokeo chanya.
Msumi amesema kwa takribani miaka sita tangu mwaka 2019 mpaka 2024 hifadhi ya taifa ya Serengeti imeshinda tuzo hiyo ambapo mambo mengi yamechagiza hifadhi hiyo kushinda ikiwemo filamu ya Royal Tour ya Mhe Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Msumi ameongeza kuwa kitendo cha serikali kuamua kuliunganisha eneo la Nyatwali kuwa sehemu ya hifadhi ya taifa ya Serengeti itaongeza idadi ya watalii lakini pia itaifanya ikologia ya wanyama kufanyika vizuri