Mazingira FM

Mbunge Maboto: “kuolewa kwa mtoto wa kike kwa sasa siyo dili waacheni wasome”

5 October 2024, 10:58 am

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto

Kipindi cha nyuma jamii nyingi za mkoa wa Mara hazikutoa kipaumbele kwa mtoto wa kike kwenda shule wakitegemea ataolewa.

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amewahimiza wazazi na walezi wilayani Bunda kuwasomesha watoto wa kike kwa kuwa kuolewa siyo dili tena.

Mhe Maboto ameyasema hayo Oct 4, 2024 katika ziara ya Mhe waziri wa Ofisi Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na utawala bora George Simbachawene wilayani Bunda wakati akizindua shule ya sekondari ya Bunda mjini.

Mhe Maboto amesema kwa kipindi cha nyuma jamii nyingi za mkoa wa Mara hazikutoa kipaumbele kwa mtoto wa kike kwenda shule wakitegemea ataolewa lakini kwa sasa kupitia jitihada za serikali ya awamu ya sita kujenga shule za msingi na sekondari kila kata, hivyo kuolewa kwa watoto wa kike siyo dili tena kwa kuwa fursa nyingi zinapatikana kama mtu ana elimu.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bunda mjini iliyozinduliwa na waziri Simbachawene Oct 4 2024

Aidha Mhe Maboto amemshukuru Mhe Rais kwa kutoa fedha katika kujenga miundombinu ya kutosha katika sekta za elimu, afya maji barabara miongoni mwa sekta zingine ambapo baadhi ya miradi hiyo kwa kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wanalazimika kuchangia

sauti ya Mbunge Robert Chacha Maboto

Katika hatua nyingine Mhe Maboto amemshukuru Mhe Rais Samia kwa kukubali kutoa fedha za kuwalipa wakazi wa Nyatwali ambapo malipo yanaendelea kutolewa kwao huku akitoa tahadhari kwa wakazi hao kuhakikisha fedha wanazozipata wanazitumia vizuri kwenda kuanzisha makazi mapya.

sauti ya Mbunge Robert Chacha Maboto