Matengenezo ya bomba kabla ya mita ya mteja ni kazi ya BUWSSA
3 October 2024, 4:36 pm
Changamoto yoyote ya matengenezo ya mtandao wa maji kwenda kwa mteja wa BUWSSA kabla ya Mita ni jukumu hilo ni kazi ya BUWSSA na matengenezo ya mteja yanahusu tu baada ya mita ya maji kwenda kwa mteja.
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa changamoto yoyote inayotokea kabla ya mita ya maji iwe kupasuka kwa bomba ni jukumu la Mamlaka ya maji kutngeneza na siyo kazi mteja.
Kauli hiyo imetolewa na Bi Esther Giryoma Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira Bunda BUWSSA wakati wa mahojiano na kipindi cha Asubuhi kupitia Radio Mazingira Fm.
Giryoma amesema changamoto yoyote ya matengenezo ya mtandao wa maji kwenda kwa mteja wa BUWSSA kabla ya Mita jukumu hilo ni la BUWSSA, na matengenezo ya mteja yanahusu tu baada ya mita ya maji kwenda kwa mteja.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za matukio kama hayo yapojitokeza ili waweze kupatiwa msaada kwa viongozi wa mamlaka hiyo akiwemo yeye kama mkurugenzi wa BUWSSA.
Mbali hilo Bi Esther amesema kufikia sasa BUWSSA wamefikia asilimia 92 ya upatikanaji wa maji Bunda na wanatarajia kufikia December 2025 wawe wamezidi lengo la serikali la asilimia 95 kwa mijini kama inavyotaja ilani ya CCM ya 2020 na 2025.
Sambamba na hilo amewatahadharisha wananchi kuwa malipo yote ya maunganisho mapya ya maji, ulipaji ankara za maji zote zinalipwa kupitia namba maalumu ya serikali (control number)