Mazingira FM

Maboto: Lazima kila mtanzania apate umeme

17 July 2024, 8:11 pm

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa uzalishaji wa umeme uliopo kwa sasa lazima kila mtanzania apate umeme kwa sababu umeme tunao wa akutosha

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto ametoa shilingi milioni 4 kwenye mtaa wa Kyaragwita kata ya Mcharo halmashauri ya mji wa Bunda.

Mhe Mbunge ametoa fedha hizo kwa ajili ya kuunga nguvu za wananchi kwenye ujenzi shule shikizi na ofisi ya serikali ya mtaa.

Mbali na fedha hizo pia Mhe mbunge anaendelea kuwataka wananchi kushirikiana na serikali kuhakikisha miradi yote inayoletwa kwenye maeneo yao inakamilika huku akiwatoa hofu wananchi kuwa wabunge wameadhimia mazuri kwenye suala la umeme.

Sauti ya Mhe Mbunge
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto akiongea na mwananchi katika moja ya mikutano ya hadhara kwenye ziara yake kata ya Mcharo, Picha na Adelinus Banenwa

Awali wananchi wakiwasilisha changamoto zao mbele ya mbunge wamesema umeme wa shilingi laki tatu na elfu ishirini ni mzigo kwao na hawana uwezo wa kulipia gharama hizo badala ya wanahitaji umeme wa shilingi elfu ishirini na saba.

Aidha kwa upande wa wakazi wa Nyabehu kata ya Guta wasemema ukosefu wa zahanati katika mtaa huo ni kilio kikubwa kwao ambapo huduma za krinik na akina mama kwenda kujifungua hutembea umbali mrefu na ikitokea wanachelewa kufika zahanati ya Guta hawapewi huduma kwa madai ya kuwa wamechelewa.

Kwa upande wa uvuvi wananchi hao wamesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya kukamatwa kwa wavuvi bila utaratibu wowote hali inayowasababishia umasikini

sauti ya wananchi