Shule ya msingi Bigutu yakabiliwa na upungufu wa madarasa
12 November 2021, 5:38 pm
Shule ya msingi ya Bigutu iliyopo kata ya Bunda stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda inakabiliwa na chambamoto mbalimbali kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosomea shuleni hapo
Akizungumza na Mazingira fm mwalimu mkuu wa shule hiyo Yohana Albert amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1761 kati yao wavulana 859 wasichana 902 huku wakiwa na maitaji ya vyumba vya madarasa 42 na vilivyopo ni 12 tu
Naye mwenyekiti wa kamati ya shule amesema anawashirikisha wazazi kuchangia maendeleo ya shule kwa kutoa michango lakini kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi bado uhitaji ni mkubwa
Kwaupande wake diwani wa kata ya bunda stoo Mh Flavian chacha amesema atashirikiana na kamati za shuleo kuangalia namna ya kushughulikia changamoto hasa kwa kuamishia nguvu kwenye shule za msingi baada ya shule za sekondari kupata ufadhiri wa fedha ya mpango wa maendeleo wa kupambana na UVICO-19 hivyo amezitaka kamati za shule kuwashirikisha wazazi kuamishia nguvu za michango kwenye shule za msingi ambazo ziko na hali mbaya
Ikumbukwe kwamba shule ya msingi ya bigutu katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2021 imeshika nafasi ya 20 kati ya shule 59 kwenye halmashauri ya mji wa bunda huku ikishika nafasi ya 299 kimkoa kati ya shule 745 na nafasi ya 6423 kitaifa kati ya shule 11909
By Adelinus Banenwa