Onyo! watumishi wasiyotoa ushirikiano kwa waandishi: RC Mtambi
19 May 2024, 1:04 pm
“Kama wewe ni mtumishi wa serikali mkoa wa Mara na hutaki kutoa habari kwa waandishi mimi nakuona ni msaliti”
Na Adelinus Banenwa
Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi ametoa onyo kwa watumishi wa serikali mkoani Mara wasiotoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kuwa wanamhujumu Rais Samia Suluhu.
kanali mtambi ameyasema hayo wakati akifunga Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari mkoani Mara yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa Mara(MRPC) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
RC Mtambi amesema kwa mtumishi wa serikali kukataa kutoa taarifa kwa waandishi angali miradi iliyotekelezwa na serikali inaonekana basi yeye anamuona kama msaliti.
Amesema, serikali ya awamu ya 6 chini ya .Rais Samia imefanya mambo mengi makubwa ya maendeleo ambayo yanatakiwa kufahamika kwa wananchi,anashangazwa na wanaoshindwa kutoa taarifa.
Awali akisoma taarifa mbele ya mkuu wa mkoa Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara Raphael Okelo amesema mkoa wa Mara una Waandishi wa Habari zaidi ya 60 na wamekuwa wakitekeleza majukumu yao licha ya changamoto mbalimbali
Amesema wanamshukuru mkuu wa mkoa na ofisi yake kwa ushirikiano wanaopata Waandishi wa Habari na kuziomba ofisi nyingine ziige mfano huo.