Mwenyekiti wa senet Mara awafunda wahitimu chuo cha ualimu Bunda
2 May 2024, 10:25 am
Suala la uzalendo, kuzingatia maadili kujituma katika kufanya kazi vyachukua nafasi nasaha za viongozi kwenye mahafali ya wanafunzi wa CCM chuo cha ualimu Bunda
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa vijana wasomi nchini kuwa na maadili mema na kufanya kazi kwa bidii ili wawe kioo kwenye jamii.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Senet mkoa wa Mara na mjumbe wa baraza la UVCCM taifa Matilda Munisi kwenye mahafali ya wanafunzi wa CCM chuo cha ualimu Bunda yaliyofanyika May 1, 2024.
Matilda amesema vijana wasomi wamekuwa na kasumba ya kusubiri ajira baada ya kumaliza masomo yao ambapo amesema wao kama vijana watumie fursa mbalimbali zinazoletwa na serikali kujitengenezea ajira badala ya kusubiri serikali.
Ametaja baadhi ya fursa hizo kama vile kuwekeza katika sekta ya kilimo, pia kutumia fedha za asilimia 10 kutoka halmashauri ambapo asilimia 4 ni kwa vijana ili ziwasaidie kujikwamua kiuchumi.
Matilda amewataka vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani kwa kuwa anaamini vijana hasa wasomi wanao uwezo mkubwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya vijana CCM wilaya ya Bunda Mohamed Msafiri amewataka wahitinu kuwa wazalendo na wenye kupendana, pia wajenge tabia ya kupeana fursa hata baada ya kutoka chuoni.
Leonard Meshack katibu hamasa CCM mkoa wa Mara amewata vijana wahitimu chuo cha ualimu Bunda na vijana wahitimu wote nchini kutafuta sifa za ziada katika kutafuta ajira kama vile kujifunza udereva computer ufundi magari miongoni mwa sifa nyingine kutokana na mahitaji ya ajira ni madogo ukilinganisha na idadi ya wanafunzi aau wataalamu wanaohitimu.
Yusuph Msuya mjumbe wa jumiya UVCCM mkoa wa Mara amewahimiza wahitimu na vijana wasomi kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kutokana na elimu waliyonayo.