Wanawake watakiwa kuachana na mikopo umiza, kausha damu
8 March 2024, 12:41 pm
Wito umetolewa kwa wanawake kuachana na mikopo kandamizi yenye riba kubwa maarufu kama kausha damu badala yake wakakope kwenye taasisi zinazotambulika kisheria kama vile benki na halmashauri.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wanawake kuachana na mikopo kandamizi yenye riba kubwa maarufu kausha damu badala yake wakakope kwenye taasisi zinazotambulika kisheria kama vile banka na halmashauri.
Hayo yamesemwa na mbunge viti maalumu mkoa wa Mara Ghati Chomete katika maadhimisho ya siku ya mwanamke dunia ambayo umoja wa wanawake wa ccm wilaya ya Bunda wameyafanya leo March 7, 2024.
Akiwa mgeni rasmi mbunge Ghati amesema ni vema wanawake katika kujikwamua kiuchumi waunde vikundi kisha wakachukue mikopo katika taasisi zinazotambulika kama vile banki yenye riba nafuu au mikopo ya halmashauri isiyo na riba badala ya kuchukuwa mikopo kausha damu ambayo inaacha fedheha na udharirishaji kwa mwanamke.
Katika hatua nyingine mbunge Ghati ametoa mabati hamsini ikiwa ni sehemu ya kuunga jitihada za umoja wa wanawake wa CCM wilaya ya bunda katika ujenzi wa nyumba ya katibu wa jumuiya hiyo.