Wanahabari watakiwa kuripoti vitendo vya ukatili dhidi ya watoto
21 October 2023, 6:47 pm
Wito umetolewa kwa waandishi habari kuripoti taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika jamii.
Na Fadhil Mramba
Wito umetolewa kwa waandishi habari kuripoti taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika jamii.
Hayo yamesemwa na afisa maendeleo mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Bi.Anna Mhina wakati akizungumza na wanahabari kutoka redio kumi na tatu za kijamii jijini Dodoma.
Amesema lengo kubwa la mafunzo ni kuwajengea uwezo wanahabari waweze kuandika habari kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto,mimba za utotoni,Magonjwa ya kuambikizwa na afya ya uzazi.
Ameongeza kuwa mpango wa serikali ni kuendeleleza mpango kazi wa kutokomeza ukatili kwa mwaka huu ambao unatokana na ule wa mwaka 2021 na wa mwaka huu utaenda hadi mwaka 2028.
Inakadiriwa watoto 246 milioni wanafanyiwa vitendo vya ukatili kila mwaka na watoto milioni 14 wapo mashuleni pia asilimia 50 ya wanafunzi wanauelewa mdogo juu ya ukatili na unyanyasaji wakijinsia.