Faru kivutio cha watalii hifadhi ya Serengeti
23 September 2023, 8:06 am
“Natoa rai kwa wananchi wote washiriki kuhakikisha kwamba Faru wanaendelea kubaki kwa ajili ya kizazi kilichopo na cha baadaye” Dkt Vincent Mashinji
Na Thomas Masalu.
Imebainishwa kuwa uwepo wa mnyama faru katika hifadhi ya taifa ya Serengeti unavutia watu wengi wa ndani na wa nje kwenda kufanya utalii katika hifadhi hiyo.
Hayo yamebainishwa leo na mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt Vincent Mashinji katika maadhimisho ya siku ya Faru Duniani yaliyofanyika Fort Ikoma wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Dkt Mashinji amesema katika kipindi cha miaka ya nyuma hifadhi ya taifa ya serengeti ilikuwa inatajwa kuwa na Faru 3 hadi leo Faru wameongezeka na kufikia zaidi ya 100.
Pamoja na hayo Dkt, Mashinji amewapongeza wale wazalendo wanaondelea kuwatunza Faru na kwamba kuruhusu kutoweka wanyama hao kunaathiri hifadhi na kukosa watalii wanaopenda kwenda kuona Faru.
Awali akitoa taarifa ya siku ya Faru Duniani, Kamishina msaidizi wa uhifadhi Albert Robson Mzirai ambaye anasimamia kitengo cha uhifadhi na maendeleo ya biashara Tanapa kanda ya Magharibi amesema haya ni maadhimisho ya 12 tangu kuanzishwa lengo ni kutoa elimu na kuelezea changamoto mbalimbali zinazokabili Uhifadhi wa wanyama aina ya Faru