BAVICHA kuadhimisha siku ya vijana duniani mkoani Mwanza
16 July 2023, 3:14 pm
BAVICHA maadhimisho ya siku ya vijana Duniani yatafanyiaka Mwanza kauli mbiu kijana ijue na itambue nguvu yako, lengo ni kuwakutanisha vijana na badarishana mawaza ya fursa zilizopo.
Na Adelinus Banenwa
Baraza la vijana chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wanatarajia kuadhimisha siku ya vijana duniani jijini Mwanza huku kauli mbiu ikiwa ni “kijana ijue na itambue nguvu yako”
Hayo yamesemwa na katibu wa baraza la vijana BAVICHA jimbo la Bunda mjini Zacharia Mbubura Ramadhani wakati akizungumza na mazingira fm ambapo amewataka vijana wa chama hicho kuhakikisha wanafika katika maadhimisho hayo kwa kuwa kuna fursa nyingi zinaweza kujitokeza.
Akizungumzia suala la vijana kukataa kujihusisha na siasa Zacharia amesema siasa ni maisha hivyo kila mtu analazimika kuingia katika mfumo huo kwa kuwa kila jambo linalofanyika linategemea maamuzi ya wanasiasa.
Ikimbukwe kwamba siku ya vijana duniani huadhimishwa kiala tarehe 12 mwezi wa nane kila mwaka ikiwa Madhumuni ya siku hiyo ni kuelekeza umakini kwenye masuala ya kitamaduni na kisheria yanayowazunguka vijana amabapo maadhimisho ya kwanza yalifanyika mwaka 2000.