Mama mwenye mtoto wa miezi miwili, akatika mguu ajali ya Basi
14 February 2023, 10:35 am
Hellena Emmanuel(23) mkazi wa Mwanza ni miongoni mwa abiria waliojeruhiwa vibaya kwenye ajali ya basi la Afrika Raha iliyotokea tarehe 12 Feb 2023 majira ya saa 9 alasiri eneo la Mwibagi Wilaya ya Butiama mkoani Mara
Akizungumza na Radio Mazingira Fm hii leo wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya DDH Bunda, Hellena amesema wakati akiwa anaendelea na zoezi la kumnyonyesha mwanaye mchanga wa miezi miwili ghafla alisikia gari linayumba na abiria wakipiga kelele na baada ya sekunde chache alijikuta wako chini ambapo yeye katika tukio hilo alikatika mguu wa kushoto huku
Katika ajali hiyo majeruhi 20 walipelekwa hospitali ya DDH Bunda ambapo kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo hadi asubuhi 13 Feb 2023 ni wagongwa 16 tu walikuwa wanaendelea na matibabu hospitalini hapo ambapo wawili waliruhusiwa kurudi nyumbani, wengine wawili walipewa rufaa ya kwenda Mwanza na kati ya waliobaki ni Helleni na mwanamme mwingine ndio waliokuwa na hali mbaya ambapo wote walikatika miguu katika ajali hiyo.