Maonesho ya Mara EXPRO yaendelea kunoga
9 September 2022, 12:25 pm
Tume ya Madini Mkoani Mara imesema tatizo la usalama wa wachimbaji wadogo wa Madini kutozingatiwa umesababisa mamlaka hiyo kufunga Baadhi ya Migodi ndani ya mkoa wa Mara
Hayo yamesemwa na Joseph Kumbulu afisa Madini Mkoa wa Mara wakati akizungumza Mazingira Fm katika maonesho ya Mara Expro yanayofanyika katika viwanja vya mkendo mjini Musoma ambapo amesema changamoto kubwa ilikuwa ni wamiliki wa mashamba kuonekana ndio wamiliki wa Madini Jambo ambalo siyo sawa kisheria
Aidha Eng Kumbulu ameongeza kuwa serikali kupitia wizara ya Madini Mkoani Mara wamefanya jitihada ya kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya uchimbaji Madini kwa kutoa elimu ambayo ilionekana ndiyo kikwazo kikubwa kwa wananchi ikiwepo namna ya utoaji vibali vya leseni za utafiti wa Madini , uchimbaji na hata pale inapotokea Mazingira ambayo si rafiki kwa wachimbaji wamekuwa wakitoa muongozo wa nini kifanyike kutatua changamoto hizo
Katika hatua nyingine Eng Kumbulu amesema tatizo la utoroshaji wa Madini wamekabiliana nalo kwa kulejesha mfumo wa kisheria ili kudhibiti vitendo vya wizi na utoroshaji wa Madini ikiwa ni pamoja kuwepo kwa Kumbukumbu kila ngazi kuanzia eneo la kuchimba, maeneo ya kuchenjulia makinikia, pia kuunda kamati kutoka eneo la mgodi kusimamia ambapo wajumbe ni viongozi wa maeneo husika wakiwepo wenyeviti wa vijiji viongozi wa wachimbaji katika Wilaya husika miongoni mwa viongozi wengine