Meja Jenerali Suleimani Mzee mkuu wa Mkoa wa Mara ajitambulisha Bunda amtaka mkandarasi anayejenga hospitali ya Halmashauri kufuata kanuni za ujenzi
18 August 2022, 10:34 am
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe Suleimani Mzee amefanya ziara katika Wilaya ya Bunda inayojumuisha Halmashauri 2 na majimbo matatu
Akimkaribisha katika ziara hiyo mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Joshua Nassar amesema kwa Wilaya ya Bunda kuna mafanikio mengi ikiwemo zoezi la utoaji elimu kuelekea zoezi la sensa ya watu na makazi, utunzaji wa Mazingira hasa utoaji wa elimu juu ya athari za ukataji miti na uchomaji wa mkaa jambo linalosababisha uharibifu wa Mazingira
Mbali na mafanikio Mhe Nassar amesema zipo changamoto zinazoikabili Wilaya ya Bunda ambapo suala la wanyapori waaribifu hasa kwa kata zilizopo Kando ya hifadhi ya Serengeti
Kwa upande wake Mhe Mkuu wa Mkoa ambaye amesema lengo kuu la ziara yake ya Leo ni kujitambulisha kama alivyofanya katika Wilaya zingine
Mbali na hayo amemshukuru mkuu wa Wilaya ya Bunda kwa kujitahidi kuanza kushughulikia changamoto na kuwa na mikakati ya kuzitatua
Katika kuendelea na ziara hiyo ya kujitambulisha Mhe Mkuu wa Mkoa amefika ofisi ya CCM Wilaya ya Bunda na kukutana na Viongozi na wanachama wa Chama hicho
Akizungumza katika ziara hiyo katibu wa CCM Wilaya ya Bunda Ndugu Loti Lazaro lemiruti amesema tayari CCM Wilaya imeshafanya uchaguzi wa Chama ngazi ya mashina matawi na kata na tayari wamepokea malalamiko kutoka kata Nne juu ya kutokulidhika na uchaguzi
Ameongeza kuwa tayari sekretarieti ya Chama imekaa kuyapitia malalamiko na tayari ameanza kuandika barua kuwajibu waliolalamika
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa amesema anashukiru kwa ushirikiano uliopo baina ya ofisi ya mkuu wa Wilaya na ofisi ya Chama
Ameongeza kuwa ushirikiano unaoonekana utumike katika kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi pia amewataka kujiandaa katika kutatua changamoto zilizopo ndani ya Wilaya ya Bunda
Pia Mhe Mkuu wa Mkoa ametembelea hospital mpya inayojengwa ya Halmashauri ya Mji wa Bunda ambayo inajengwa eneo la bunda stoo
Thamani ya majengo mawili yanayojengwa kwa sasa ni million 500
Mhe mkuu Mkoa amemtaka mkandarasi kusimamia ujenzi kama alivyofundishwa na kufuata utaratibu wote wa ujenzi huku akielekeza kuwepo kwa Kumbukumbu za nyaraka zote za manunuzi na ziwepo site muda wote
Kuwepo kwa bango ambalo linaonesha maendeleo ya ujenzi katika kila hatua ya ujenzi