Maandalizi ya “Bunda Nyamachoma festival” usipime
5 November 2024, 11:40 am
Zitakuwepo burudani mbalimbali zikiongozwa na msanii wa singeli Dullah Makabila, pamoja na vikundi vingine vingi kutoka mkoa wa Mara
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Bunda kujitokeza kwa wingi katika tamasha la uchomaji wa nyama (Bunda nyama choma festival) unaotarajiwa kufanyika siku ya ijamaa tarehe 8 Nov 2024 katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Bunda
Akizungumza ndani ya kipindi cha Asubuhi leo kupitia studio za radio Mazingira fm kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bunda dkt Vicent Anney, katibu tawala wilaya ya Bunda Ndugu Salum Halfani Mtelela amesema lengo la tamasha hilo ni kuitangaza nyama ya mkoa wa Mara ilivyo na ubora kuliko za maeneo mengine
Aidha ameongeza kuwa tamasha hilo pia litahusisha shughuli zingine ikiwemo matembezi ya amani yaani jogging asubuhi ambayo itaanzia kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya na itaishia stendi ya zamani pia zitakuwepo burudani mbalimbali zikiongozwa na msanii wa singeli Dullah Makabila, pamoja na vikundi vingine vingi kutoka mkoa wa Mara
Katibu tawala huyo amesema katika tamasha hilo hakuna kiingilio isipokuwa ni wewe kufika eneo la stendi ya zamani mjini Bunda kuanzia asubuhi na fedha yako ambayo itakusaidia kula nyama kadri uwezavyo ambapo washindi wa kuchoma nyama nafasi ya kwanza hadi ya tatu mbali na zawadi watakazopata pia watapata nafasi ya kupata tiketi za bure kushiriki kwenye mbio za Serengeti safari Marathon
Iikumbukwe tamasha hilo la Bunda Nyama choma Festival mgeni rasmi atakuwa ni mkuu wa mkoa wa Mara Mhe Kanal Evance Mtambi.